Mwaka 2015 ulikuwa mwaka mzuri wa maendeleo ya sayansi na teknolojia kwenye vyombo vya habari kupitia simu za mkononi ambapo mtandao wa Instagram ulipata umaarufu zaidi duniani kwa kuweka picha.
Mtandao huo umetoa orodha ya picha zilizopata ‘Likes’ nyingi zaidi duniani ambapo picha ya mwanafamilia wa The Kardashians, Kendall Jenner imetajwa kuwa picha ambayo ilipata kupendwa zaidi na watumiaji wa mtandao huo. Ilipata ‘Likes’ milioni 3.2.
Picha hii iliwekwa Desemba 2 mwaka jana.

Kendall Jenner
Nafasi ya pili imechulikuwa na picha ya Tailor Swift akiwa karibu na ua iliyopostiwa na Kanye West. Ilipata Likes Milioni 2.6.
Picha nyingine ya Tailor Swift akiwa amebebwa mgogoni na mpenzi wake, DJ Calvin Harris ilishika nafasi ya tatu kwa kuwa na likes milioni 2.6.
Nafasi ya nne ni picha ya Kylie Jenner akiwa anawaonesha mashabiki wake cheti cha kuhitimu elimu ya stashahada. Picha hiyo ilipata Likes milioni 2.3.
Beyonce akiwa na mwane Blue Ivy walivutia Likes milioni 2.3 na hivyo kushika nafasi ya tano kati ya zilizopendwa zaidi.