Dj maarufu nchini, Hyperman HK anatarajia kuwa mshenga katika ndoa ya mkali wa miondoko ya Singeli, Dulla Makabila na msanii wa Bongo movie, Husna Sajent waliokuwa kwenye uhusiano wa mapenzi kwa muda mrefu.

Hyperman ambaye hivi karibuni alikuwa gunzo baada ya kufahamika alikuwa Mshenga wa ndoa ya msanii wa Bongo Fleva, Nuh Mziwanda na mpenzi wake Nawar ambao waliachana hivi karibuni, amesema hafurahishwi kuona watu aliowaunganisha wanaachana ndani ya muda mfupi.

Akizungumza kupitia E-News ya EATV, Hyperman amesema ndoa zinazokaa kwa muda mfupi zinasababishwa na watu kutoshibana na wakati mwingine kuingia kwenye ndoa wakati wa umri mdogo

“Mimi inaniuma sana ninapokuwa mshenga halafu ndoa inavunjika wakati hawajapata hata watoto wawili au watatu…hainifuraishi hata kidogo watu ninaowaunganisha kuachana,’’ Hyperman alifunguka.

Akizungumzia ndoa ambayo anatarajia kuisimamia ya Dulla Makabila na Husna Sajent, HK amesema anaamini ndoa hiyo itadumu kwani wawili hao wamekuwa wakielewana vizuri katika kipindi ambacho wamekuwa wapenzi.

‘’Hii ndoa itakaa kwa muda mrefu sasa kwasabu kwanza wamekaa kwa muda mrefu sana kwenye mahusiano na naona wanaelekea sehemu salama’’ amesema Hyperman.

Dulla Makabila ambaye anatamba hivi sasa na wimbo wake wa ‘Hujaulamba’ amekuwa akionekana kwenye picha akijivinjali na mpenzi wake, Husna Sajent ambae amezaa na msanii wa muziki wa dansi, Chaz Baba.

Serikali yalipongeza Shirika la Utangazaji Tanzania (TBC)
Kenyatta aishangaza Dunia, aingia kwenye rekodi ya pekee