Kocha mkuu wa timu ya taifa ya England, Roy Hodgson ameshindwa kutaja kikosi kitakacho pambana katika michezo ya kuwania kufuzu fainali za mataifa ya barani Ulaya za mwaka 2016.

Hodgson, amechelewa kufanya hivyo kwa kuhofia majeraha kwa wachezaji wake ambao wanaendelea kuzitumikia klabu zao kwenye ligi ya nchini humo.

Hodgson, amekua akishuhudia baadhi ya michezo ya ligi ya nchini England kwa lengo la kuwafanyia tathmini wachezaji ambao anahisi wanafaa kuwa sehemu ya kikosi chake ambacho kitapambana dhidi ya San Marino pamoja na Uswiz mwanzoni mwa mwezi ujao.

Kufika viwanjani mara kwa mara kwa kocha huyo, kuliwaaminisha wadau wa soka nchini humo, huenda angewahi kutaja kikosi cha timu ya taifa lakini imekua tofauti mpaka sasa.

Alipoulizwa na waandishi wa habari kwa nini amechelewa kufanya hivyo, Hodgson alijibu lengo lakle kubwa ni kutaka kuwa na wachezaji wenye utimamu wa mwili na si kuwa na mtu ambaye atashindwa kufikia lengo la kucheza kwenye michezo hiyo inayowakabili.

Amesema anahitaji kuwa na kikosi imara hata kama baadhi ya wachezaji hawatokuwepo kutokana na hofu yake ya kuwa majeruhi, lakini akasisitiza dhahir hitaji lake la kutaka kuona kila mmoja atakaemuita kikosini anakua sawa sawa kwa mapambano.

 

Tayari kuna shaka kwa wachezaji wa Liverpool, Jordan Henderson na Adam Lallana, kutokuwepo kwenye kikosi cha England pamoja na kiungo wa Man City, Fabian Delph kufuatia majeraha yanayowakabili kwa sasa.

Henderson na Lallana walikosa mchezo wa usiku wa kuamkia hii leo dhidi ya Arsenal kutokana na hali zao kimwili kutokua nzuri.

Balotelli Awasili Mjini Milan
ACT- Wazalendo Kuzindua Kampeni Jumapili