Ujerumani imerekodi maambukizi mapya 33,949 ya Covid19 ndani ya siku moja ikiwa ni 172% kuzidi rekodi za desemba 2020.

Rais wa Taasisi ya Kudhibiti Magonjwa ya Kuambukiza nchini humo Robert Koch amesema inawezekana wimbi la 4 kuja kwa kasi kwa sababu wasiochanjwa na wanaopuuza sheria ndio wabebao virusi.

Wakati huo huo, Ubalozi wa Marekani Nchini Tanzania umewakumbusha Raia wote wa kigeni ambao ni Watu wazima wataosafiri kwenda Marekani kwa njia ya anga kuanzia Jumatatu ijayo tarehe 8 Novemba watatakiwa kuonesha uthibitisho kuwa wamepata chanjo kamili ya covid 19.

Pamoja na hilo pia atatakiwa kuonesha cheti kinachoonesha kwamba hana maambukizi ya covid 19 baada ya kufanya kipimo ndani ya siku tatu zilizopitaa

Habari kubwa kwenye magazeti leo, Novemba 5, 2021
Matabibu mtarudia mitihani:Mganga Mkuu Sichalwe