Wakati serikali ya kenya ikiendelea kupambana na wanamgambo wa kiislamu wanaoishambulia nchi hiyo kwa nyakati tofauti tofauti Mashirika ya ujasusi nchini Kenya yanakadiria kwamba huenda takriban wanaume na wanawake 100 wakawa wamekwenda kujiunga na kundi la Dola la Kiislamu nchini Libya na Syria.
Imebainika kwamba  ushawishi wa kundi la Dola la Kiislamu Afrika Mashariki umeongezeka kwa kuwaandikisha vijana wa Kenya kuendesha mapambano ya jihadi nchi za nje na baadhi yao kurudi Kenya kuitishia nchi hiyo kufanya mashambulizi kwa Kenya na katika vituo vya kigeni
Rashid Abdi mchambuzi mwandamizi katika Shirika la Kimataifa la Kushughulikia Mizozo ambalo ni jopo la ushauri lilioko katika mji mkuu wa Kenya Nairobi amesema “kwamba hivi sasa kuna tishio la kweli linaloikabili Kenya kutoka kundi la Dola la Kiislamu na hatari hiyo itazidi kuongezeka.
Aidha Polisi  nchini humo ilisema imegunduwa vitu ambayo hutumiwa na magaidi kutengeneza mabomu ya kienyeji pamoja na mikuki na mishale iliotiwa sumu.
Baadhi ya wataalamu  Kenya wanakiri kwamba kuna tishio la dhati la kundi la Dola la Kiislamu kupandikiza itikadi kali, kuandikisha watu kujiunga nalo na baadae kuwarudisha nyumbani
Kenya tayari ni muhanga wa mashambulizi ya kigaidi yanayofanyika kila mara nchini humo na sasa imekuwa katika wasiwasi kwamba vijana wazawa wa nchi hiyo wataweza kuishambulia baada ya kugundulika kwa baaadha yao kujiunga na kundi hilo la kigaidi.
                DW

 

Themi Felix Asajiliwa Tena Kagera Sugar
Vicente Del Bosque Atangaza Kujiuzulu