Afrika Magharibi inakabiliwa na wimbi jipya la maambukizi ya homa ya Ebola tangu mlipuko mbaya wa homa hiyo ulipomalizika mwaka 2016 baada ya kugundulika visa vipya saba Februari 14,2021, ambapo Mkuu wa afya wa Guinea ameviita kuwa ni janga.

Licha ya janga la COVID-19 kuchukua sehemu kubwa ya rasilimali za afya za Guinea, lakini taifa hilo na shirika la afya ulimwenguni (WHO), wanasema wamejiandaa vyema kukabiliana na Ebola kwa wakati huu kuliko ilivyokuwa miaka mitano iliyopita kwa sababu ya hatua zilizopigwa kwenye eneo la chanjo.

WHO imesema itapeleka haraka msaada wa chanjo nchini Guinea na kuhakikisha inapata kiwango cha kutosha, wakati mataifa jirani Liberia na Sierra Leone wakichukua tahadhari kubwa kama hatua za awali za kujilinda.

Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo wiki iliyopita ilitangaza kurejea kwa homa hiyo, ikiwa ni miezi mitatu tangu mamlaka zilipotangaza kumalizika kwake.

Nchi za Magharibi zaitaka Myanmar kutotumia nguvu
Mwenyekiti wa BBI afariki dunia