Wananchi wa kijiji cha  Muungano wilayani Momba mkoa wa Songwe wameyakimbia makazi yao wakihofia kukamatwa baada ya kuwapo kwa msako wa kuwakamata wasiokuwa na vyoo.

Kata ya Kamsamba ni miongoni mwa kata ambayo imekubwa na ugonjwa wa mlipuko wa kipindupindu kilichosababisha watu zaidi ya 100 kuugua.

Hivyo Serikali imeamua kuweka mkakati ili kudhibiti ugonjwa huo.

Afisa Mtendaji wa kata ya Kamsamba, Gerald Makwasa amesema viongozi ngazi ya wilaya wakiwa na mgambo walifika katika bonde la kamsamba kuendesha msako wa kuwasaka wasiokuwa na vyoo hali iliyowalazimu wakazi wa kijiji hicho kukimbilia kusikojulikana.

Afisa Tarafa ya Kamsamba amesema siku chache zilizopita walikaa kikao na mganga mfawidhi wa kituo cha afya cha Kamsamba kujadili hali hiyo ambapo alisema kata zizokumbwa zaidi ni Ivuna yenye wagonjwa 35, samang’ombe 35, na kasmaba yenye wagonjwa 34 huku mmoja kufariki dunia.

Amesema ugonjwa huo uliibuka Novemba 11, 2018 ambapo jitihada mbalimbali zilifanyika kudhibiti hali hiyo.

”Ni kweli wananchi karibu wote kijiji cha Muungano wameyakimbia makazi yao wakihofia kukamatwa, lakini tumeandika majina yao, tunafahamu kuwa watarejea tu kwani wameacha familia zao wengine wake zao ni wajawazito amesema Mwasomola.

Aidha, Mkuu wa Wilaya hiyo, Juma Irando amesema oparesheni hiyo ni endelevu ya kuhakikisha kila kaya inakuwa na choo bora.

Kigwangalla aibukia sakata la Fastjet kunyimwa vibali
Video: Mbowe atuma ujumbe mzito kutoka Segerea, ATCL yampa JPM majina ya vigogo