Serikali kupitia Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto imetoa tahadhari kwa wananchi juu ya kuingia kwa ugonjwa wa Dengue na kutoa taarifa kwa umma kuwa bado ugonjwa wa homa wa Dengue upo hapa nchini licha ya kuwa mpaka sasa hakuna kifo kilichotokana na ugonjwa huo.

Naibu Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk. Faustine Ndungulile amesema kuwa serikali inatoa taarifa ya kuwepo kwa ugonjwa wa homa ya dengue hapa nchini na ugonjwa huo umeibuka tena na kuendelea kuthibitishwa nchini hususani katika majiji ya Dar es Salaam na Tanga kuanzia mwezi Januari 2019.

Ameongezea kwamba hadi kufikia terehe 2 Aprili 2019 kati ya watu 470 waliopimwa wagomjwa 307 wamethibitishwa kuwa na virusi au walishapata ugonjwa wa homa na kati yao hao 252 kutoka Dar es Saalam na 55 wanatoka Tanga.

“Katika jiji la Dar es Salaam wagonjwa wamethibiitishwa katika hospitali ya Mwananyamala, Ilala, Temeke, Vijibweni, Aga-Khani, Regency, IST na Ebrahim Haji.

“Kutoka katika jiji la Tanga wagonjwa wamethibitishwa katika hospitali za Bombo, Aga-Khan, Burhan Street 4 na Safi Medics,” alieleza Dk. Ndungulile.

Aidha alieleza kuwa ugonjwa huo siyo ugonjwa mpya nchini na katika miaka ya 2010, 2013,2014 na 2018 hasa ukizingatiwa uwepo wa mbu ambaye anaeneza ugonjwa huo.

Video: Mifuko ya Plastiki yapigwa marufuku | Mbadala wapatikana
Breaking News: Rais wa Sudan aliyetawala miaka 30 ang'olewa madarakani

Comments

comments