Baada ya kuwa kimya kimuziki msanii wa Bongo fleva Estelinah Peter Sanga, maarufu kama Lina Sanga, mapema leo hii amejifungua mtoto wa kike katika hospitali ya Maria Stopes iliyopo jijini Dar es salaam maeneo ya mwenge.

Inasemekana mimba yake ilipitiliza muda wake, lakini kwa sasa hilo sio swala kwani leo hii amemleta mwali.

Kabla ya kupata ujauzito kutoka kwa baba mtoto wake anayejulikana kama director Ghost, huko nyuma Linah aliwahi kupata misukosuko baada ya mimba aliyopewa na mpenzi wake wa zamani kutoka.

Ila leo hii Linah amewafanyia furaha wengi kuleta kiumbe duniani.

Wasanii mbalimbali kupitia mitandao ya  kijamii wametumia akaunti zao kumpongeza Linah kwa kujifungua salama mtoto wa kike.

Hadi sasa Linah hajapost chochote kwenye mitandao yake ya jamii.

Pete ya ukeni inayozuia virusi vya ukimwi kufanyiwa majaribio Afrika
Wanasheria na wakaguzi wa mazingira wapigwa msasa