Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam, Paul Makonda, mapema leo hii Julai 17, 2018 amepata mtoto wa kiume kutoka kwa mke wake wa ndoa Maria Makonda.

Mtoto huyo wamempa jina la Keagan Paul Makonda.

Wasanii, wanasiasa pamoja na watu maarufu mbalimbali wametumia kurasa zao kutoa pongezi za dhati kwa familia hiyo kwa kufikia hatua hiyo.

Aidha katika ukurasa wa Instagram wa Mkuu wa Mkoa, Paul Makonda ameandika.

” Mungu wewe ni wa ajabu, unatenda kwa wakati wako, Asante kwa zawadi ya mtoto wa kiume @Keagan P Makonda.

Naye mke wa Nyalandu, Faraja Nyalandu katika ukurasa wake wa Instagram ameandika

” Maria na Paul nilishuhudia mkiapa kiapo cha ndoa takatifu na leo nashuhudia mkiwa baba na mama Keagan. Hakika Mungu wetu ni mwaminifu njia zake sio kama zetu, kama mbingu zilivyo juu ndivyo mipango yake ilivyo juu  ya waaminio” Faraja Nyalandu.

Dar24 Media inatoa pongezi za dhati kabisa kwa familia ya Mkuu wa Mkoa Paul Makonda kwa kuongeza jembe @”Keagan.

Man Utd kujitosa kwa Ivan Perisic, Ante Rebic
Video: IGP Sirro aje ofisini aniambie, Jeshi la Polisi limenyoosha mikono kwa Majambazi?- Lugola

Comments

comments