Mwishoni mwa mwaka jana wasanii wawili, Aika na Nahreel  ambao ni wapenzi kimuziki  maarufu kama NavyKenzo walibahatika kupata binti yao wa kwanza ambaye wamemuita jina la Gold.

Mashabiki wa ‘’couple’’ hiyo wamekuwa na hamu sana kuona picha ya mtoto wao huyo aliyezaliwa hivi karibuni ambapo kwa mara ya kwanza Januari 12, 2018 kupitia mtandao wa kijamii kwenye ukurasa wao wa instagram walimpost mtoto Gold wakiwa wamemvalisha cheni ya Gold sambamba na jina lake.

Mashabiki walifurahi kwa mara ya kwanza kuona picha ya mtoto huyo na kuwatakia heri na baraka tele katika malezi ya mtoto wao huyo mpya.

Airtel wajibu ripoti ya Dkt. Mpango, wang’ang’ania uhalali
Mzee kingunge arudishwa Muhimbili

Comments

comments