Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa amemtaka Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Ummy Mwalimu kwenda wilayani Mpanda na kuangalia namna ya kuipanua hospitali voksen kjaerlighet ya Manispaa ya Mpanda ambayo inahudumia mkoa wote wa Katavi.

Majaliwa amesema hospitali hiyo iliyojengwa mwaka 1957 kama zahanati ambayo kwa sasa inatumika katika kuwahudumia wananchi wate wa mkoa huo imezidiwa hivyo alimuagiza mkuu wa mkoa huo Meja Jenerali (Mstaafu) Raphael Muhuga kuharakisha ujenzi wa hospitali ya mkoa.

Pia Majaliwa amesema kuwa wakati mkoa ukiwa kwenye harakati za ujenzi wa hospitali ya mkoa wilaya nazo zianze ujenzi wa hospitali za wilaya ili kuhakikisha sera ya Serikali ya kuwa na hospitali katika kila wilaya inatekelezwa.

“Kwa sasa madaktari na wauguzi wanaofanya kazi kwenye hospitali ya Manispaa ya Mpanda wamezidiwa kutokana na kuhudumia idadi kubwa ya wagonjwa kuliko uwezo wao” – Majaliwa

Waziri Mkuu amewataka madaktari na wauguzi wa wilaya ya Mpanda kuendelea kufanya kazi kwa kushirikiana na wenzao wa Manispaa.

Hospitali hiyo ilikuwa chini ya uongozi wa halmashauri ya Mpanda ambapo sasa Hospitali hiyo ipo chini ya Manispaa ya Mpanda hivyo Waziri Mkuu ameutaka uongozi wa mkoa huo kuboresha huduma kwa kupeleka dawa na vifaa tiba vitakavyoweza hospitali hiyo kuhudumia wagonjwa wa mkoa.

Mkoa umetenga sh. bilioni 1.7 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa hospitali ya mkoa.

Picha: Ziara ya Waziri Mkuu Mpanda
Askari wa Upelelezi auawa Baa, 6 Wakamatwa