Hospitali ya Nairobi nchini Kenya imekanusha kuhusika na kifo cha mwanamke mmoja aliyefanyiwa upasuaji wa kuongeza matiti mara tatu.

Hospitali hiyo imesema kuwa binti huyo, June Wanza alifika katika hospitali yao mara baada ya kupata shida iliyotokana na upasuaji aliofanya katika kliniki moja nchini humo.

”Nathibitisha kifo cha binti huyo kutokea hospitali ya Nairobi ambapo alikuja kwa ajili ya uchunguzi na matibabu zaidi mara baada ya kupata shida iliyotokana na kufanyiwa upasuaji aliofanywa na madaktari watatu tofauti na kwa mara tatu’ amesema Dkt. Christopher Abeid wa Hospitali ya Nairobi.

Aidha, taratibu za uchunguzi zikiwa zinaendelea kufanywa na vyombo husika vya dola nchini Nairobi, Mahakama katika uchunguzi wake ilimgundua mmoja wa madaktari, Dkt Ajujo aliyehusika na upasuaji wa binti kuwa hakuwa na vigezo vya kumfanyia upasuaji.

Mahakama katika uchunguzi wake ilibaini kuwa daktari huyo alikuwa katika mafunzo ya vitendo hivyo hakupaswa kufanya upasuaji huo bila kuwa na usimaizi kutoka kwa mkuu wa kitengo cha upasuaji, ambapo yeye alivunja utaratibu huo na kumfanyia upasuaji binti huyo.

Hata hivyo Hospitali ya Nairobi imepeleka mbele kesi hiyo ili mahakama iweze kusikiliza na kutolea uamuzi juu ya chanzo ha kifo cha binti huyo. june Wanza.

 

Video: Vigogo CCM wamtega Magufuli, Mmiliki mwendokasi kortini tuhuma nzito
Urusi yajipanga kuzima Intaneti ili kujilinda na maadui