Naibu Waziri wa Afya Dkt Godwin Mollel ameagiza Hospitali za Rufaa za Mikoa zilizopo pembezoni mwa nchi kuweka utaratibu endelevu wa kuwa na kambi za kutoa huduma za kibingwa kwa wananchi.

Dkt Mollel ametoa agizo hilo leo Januari 26, 2022 wakati wa uzinduzi wa Kambi ya Huduma za Kibingwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa Maweni Kigoma na kujionea hali ya utoaji wa huduma kwa wananchi.

“Huu utaratibu wa madaktari wetu bingwa kutoka hospitali za kibingwa kuwafuata wananchi waliopo kwenye Mikoa iliyopo pembezoni na kuhudumiwa huko utakuwa ni utaratibu endelevu na kwa maeneo yote ya pembezoni katika nchi yetu” amesema Dkt. Mollel

Ahmed Ally: Tutaonesha soka letu Kaitaba
Hassan Mwakinyo akanusha kuvuliwa Ubingwa