Operesheni ya kubomoa nyumba zilizojengwa katika maeneo ya wazi, maeneo ya mabondeni na maeneo yaliyo umbali usioruhusiwa kisheria kutoka barabarani imezisomba hoteli maarufu jijini Dar es Salaam, Double Tree na Slipway.

Serikali imewapa wamiliki wa hotel hizo siku saba kuhakikisha wanazibomoa hotel hizo vinginevyo itazibomoa na kuwadai kulipia gharama za kubomoa. Zoezi la kuweka alama ya X pia limeikuta nyumba ya tajiri Maheshbhai Patel pamoja na nyumba nyingine za vigogo zilizojengwa karibu na barabara ya Slipway, Msasani Peninsula.

 

Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, William Lukuvi alisema kuwa serikali itaendelea kusimamia sheria bila kujali watu ambao wanaonekana kuwa na jeuri ya pesa.

Alisema kuwa baadhi ya wamiliki wa nyumba zilizoko katika maeneo hayo walipewa kibali na serikali kupendezesha maeneo yaliyo pembeni mwa barabara kwa kupanda maua na kufunga minyororo lakini wao wakakiuka na kujenga ukuta.

“Wangependezesha na kufunga minyororo kama walihofia kuharibiwa mazingira yao kama walihisi wananchi wangeharibu, lakini sio kujenga ukuta. Nimeagiza Kinondoni kuwapatia notisi ya siku saba kubomoa kwa hiari. Wasisubiri serikali ije kuvunja,” alisema Waziri Lukuvi.

Ibrahim Ajib Awapa Zawadi Ya Mwaka Mpya Mashabiki Wa Simba
Kagame atoa tangazo rasmi la Utawala wa Muhula wa Tatu