Mjasiliamali na mwanamitindo maarufu nchini Kenya, Huddah Monroe amemtaka Rais wa nchi hiyo Uhuru Kenyatta kuhalalisha bangi .

Huddah ameomba mtu aliyekaribu na Kenyatta kumfikishia ujumbe huo kuwa kabla ya kura ya maoni Rais Kenyatta ahalalishe matumizi ya kilevi hiko kinachotumiwa na vijana wengi nchini humo.

Huddah kupitia ukurasa wake wa instagram ameandika.

“Kabla ya kura ya maoni, tunataka bangi ihalalishwe. Ni nani aliye karibu na rais kwa sasa? Mfikishieni ujumbe huu.”

2017, hoja hiyo iliungwa mkono na Wakenya zaidi ya 1,400 mara baada ya mtafiti Gwada Ogot kuwasilisha ombi lake mbele ya Bunge la Senet na kubainisha kwamba matumizi ya bangi kiafya yana faida nyingi ikiwemo kusaidia kuimarisha hali ya uchumi nchini.

Aidha, sheria nchini Kenya inapiga marufuku utumiaji wowote wa bangi na kwamba mtu yeyote atakayepatikana akitumia dawa hiyo atashtakiwa kwa uhalifu.

Mtafiti Gwadahuyo alikiri kuvuta bangi wakati alipokuwa kijana,  amesema kuwa mataifa mengi katika bara Ulaya na Asia  na majimbo kadhaa nchini Marekani yamehalalisha utumiaji wa marijuana.

Ameorodhesha pia nchi za Colombia, Mexico, Jamhuri ya Czech, Costa Rica, Ireland, Australia, Jamaica na Ujerumani miongoni mwa nchi zilizohalalisha matumizi ya bangi.

Video: Dkt. Kihamia afunguka kuhusu uchaguzi wa marudio Liwale
Video: Ngoma ya Ney wa Mitego 'Alisema' yakumbushia utata kifo cha Akwilina