Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman, amesema suala la upatikanaji wa huduma bora kwa Watu Wenye Ulemavu nchini, sio la hiari bali ni la matakwa ya katiba ambayo yanapaswa kusimamiwa vyema katika utekelezwaji wake.

Othman, ameyasema hayo katika Uwanja wa Gombani ya Kale Chake Chake Pemba wakati wa Kilele cha Siku ya Watu Wenye Ulemavu Duniani, ikiwa ni hatua ya kutathimini juhudi mbali mbali zinazofanyika kitaifa na kimataifa katika kulinda haki na utolewaji wa fursa sawa kwa watu wenye ulemavu.

Amesema, kutokana na hali hiyo serikali zote mbili zimekuwa zikichukua hatua na jitihada mbali mbali kukabiliana na kuondosha changamato tofauti zinazowakabili Watu Eenye Ulemavu ingawa bado zinaendelea kuwakabili.

Miongoni mwa changamoto hizo ni pamoja na upungufu wa walimu na vifaa katika elimu mjumuisho , uhaba wa huduma na vifaa vya marekebisho kwa watu wenye ulemavu pamoja na kuwepo miundombinu isiyorafiki na uhaba wa wataalamu wa lugha ya alama ,suala la uwezeshaji wa kiuchumi pamoja na udhalilishaji hasa watu wenye ulemavu wa akili.

Makamu wa Kwanza wa Rais wa Zanzibar, Othman Masoud Othman.

Hata hivyo, ameitaka jamii kubadili mfumo wao wa maisha hasa katika ulaji wa vyakula mbali mbali kwa kuachana na vyakula vya mafuta
kwa wingi pamoja na uwanga ili kupunguza uwezekano wa kupata maradhi yasiyoambukiza ambayo pia husababisha ulemavu na pia kuwa na tabia ya kuchunguza afya zao mara kwa mara.

Kwa upande wake, Waziri wa Nchi Afisi ya Makamu wa Kwanza wa Rais Zanzibar, Harous Said Suleiman, ameitaka jamii kuacha kuwaficha watoto wenye ulemavu kwani kufanya hivyo ni kuwanyima haki zao huku Mwenyekiti wa Baraza la Watu Wenye Ulemavu Zanzibar Bi Salma Saadat amesema kwamba Watu Wenye Ulemavu wanapaswa kufunzwa na kuibua vipaji vyao vya aina mbali mbali walivyonavyo ili waweze kuendelezwa.

Dkt. Samia apewa tuzo mafanikio sekta binafsi
Askari waliotimiza miaka 22 kazini watoa msaada