Mlinda mlango wa timu ya taifa ya Ufaransa, Hugo Lloris amegoma kusaini mkataba mpya wa kuendelea kuitumikia klabu ya Tottenham Hotspurs, baada ya kutakia kufanya hivyo kabla ya kuanza kwa fainali za Euro 2016.

Spurs tayari ilikua imeshamuandalia Lloris mkataba wa miaka mitano, na kabla ya kumtaka ausaini walikaa chini na kuzungumza baadhi ya mambo lakini cha kushangaza aligoma kutimiza jambo hilo.

Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 29, amekua akihusishwa na taarifa za kuwindwa na klabu bingwa nchini Ufaransa Paris Saint-Germain, na inahisiwa huenda hatua ya kukataa kwake kusaini mkataba mpya ni kutaka kushinikiza dili la uhamisho wake likamilike.

Hata hivyo uongozi wa Spurs, unaamini bado kuna nafasi nyingine ya kukaa chini ya Lloris kwa ajili ya kufanya mazungumzo upya ya mkataba wake, ili afanikishe hatua za kuusaini.

Meneja wa klabu hiyo ya kaskazini mwa jijini London, Mauricio Pochettino amedhamiria kubaki na wachezaji wake wote waliofanikisha azma ya kutinga kwenye michuano ya ligi ya mabingwa barani Ulaya msimu ujao, hivyo anatarajia kuwa sehemu ya wapambanaji watakao mshawisho Lloris akubalia kusaini mkataba mpya.

Everton Wakorogana, Kila Mmoja Anamtaka Kocha Wake
Euro 2016: Pele Amtumia Salamu Marcus Rashford