Mlinda mlango kutoka nchini Ufaransa Hugo Lloris amesisitiza kuendelea kuitumikia klabu yake ya Tottenham Hotspurs.

Lloris amesisitiza mpango huo, huku mkataba wake ukitarajia kufikia kikomo mwaka 2019, na mpaka sasa hakuna tetesi zozote za kusaini mkataba mwingine.

Lloris amesema bado ana uheshimu mkataba alionao kwa sasa, na hafikirii nini kitakachojitokeza baadae, kutokana na kufahamu wajibu wake klabuni hapo.

Amesema litakua jambo la kipuuzi kwake kudai mkataba mpya wakati bado ana uthibitisho wa kuwa mchezaji halali kwa kipindi cha miaka mingine miwiwli ijayo.

Mlinda mlango huyo mwenye umri wa miaka 29, amekua akihusishwa na taarifa za kurejea nyumbani kwao Ufaransa, huku klabu bingwa nchini humo Paris Saint-Germain ikitajwa kusuka mipango ya kumsajili.

Lloris alijiunga na Spurs mwaka 2012 akitokea Ufaransa alipokua akiitumikia Olympique Lyonnais, na mpaka sasa ameshaidakia klabu hiyo ya jijini London katika michezo 140.

Rais Malinzi Akumbuka Ukarimu Wa Shekiondo
Uamuzi Wa Kamati Ya Saa 72 Ya Uendeshaji Na Usimamizi Wa Ligi