Hukumu ya aliyekuwa Waziri wa Fedha, Basil Mramba, aliyekuwa Katibu Mkuu wa Wizara ya Fedha, Gray Mgonja na aliyekuwa Waziri wa Nishati na Madini, Daniel Yona wanaokabiliwa na mashtaka ya matumizi mabaya ya madaraka na kuisababishia serikali hasara ya Shilingi bilioni 11.7 imeahirishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu jijini Dar es Salaam hadi Julai 3, mwaka huu.

Akitoa taarifa ya kutokuwepo kwa hakimu huyo, mmoja wa mahakimu wanaounda jopo hili, Jaji John Utamwa alisema kwamba Hakimu Kinemela yupo mkoani Dodoma kwa shughuli maalum za kibunge hivyo hawawezi kutoa hukumu hiyo bila jopo hilo kukamilika.

Makamba: Anayemwaga Fedha Kusaka Urais Hafai
Usain Bolt Awapa Ahuweni Wapinzani Wake
Tags