Maombi ya zuio la muda la ubunge wa waliokuwa wanachama wa Chadema 19 wa Viti Maalum, waliovuliwa uanachama wa chama hicho yanaanza kusikilizwa leo Jumatatu, Mei 16, 2022 na Jaji John Mgetta katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam

Zio hilo ni dhidi ya Bodi ya Wadhamini wa Chadema, Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) na Mwanasheria Mkuu wa Serikali (AG), yanasikilizwa leo.

Wanachama hao wa zamani wa Chadema, Halima Mdee na wenzake 18 walivuliwa rasmi uanachama wa chama hicho, usiku wa kuamkia Mei 12, 2020, baada ya Baraza Kuu la Chadema kutupilia mbali rufaa zao walizozikata wakipinga uamuzi wa Kati Kuu iliyowavua uanachama.

Baraza Kuu la Chadema, ambalo ndilo chombo cha juu kabisa cha maamuzi ya Chadema lenye uamuzi wa mwisho katika kikao chake hicho liliunga mkono uamuzi wa Kamati Kuu.

Kamati Kuu ya Chadema iliwavua uanachana Novemba 27, 2020, ilipowatia hatiani kwa kosa la kwenda kuapishwa kuwa wabunge wa viti maalum kinyume cha utaratibu wa chama.

Huko Bungeni wabunge hao wameonekana kuhudhuria vikao vya Bunge na Spika wa Bunge, Tulia Ackson amesema anasubiri uamuzi wa mahakama kuhusu wabunge hao na wataendelea na ubunge mpaka pale uamuzi wa mahakama utakapotolewa.

Katika maelezo yake, Dk Tulia amesema kuwa amepata taarifa kutoka kwa wabunge hao kuwa tayari wameshafungua kesi  Mahakama Kuu ya kupinga mwenendo wa kuvuliwa uanachama na Kamati Kuu na baadaye Baraza Kuu kukataa rufaa yao.

“Bunge haliwezi kuingilia mchakato huo mpaka Mahakama Kuu itakapotoa uamuzi, ninalazimika kutokutangaza kuwa nafasi za viti maalumu 19 vya Chadema viko wazi mpaka pale mahakama itakapokamilisha kazi yake ya kutoa uamuzi” amesema Dk Tulia

Spika amekiri kupokea barua za pande mbili ikiwemo ya Chadema ambao walimtaarifu kuhusu kuwafukuza uanachama wabunge hao 19 wa Viti Maalum.

Nyingine ni barua ya wabunge hao ambayo inaeleza kuwa wamefungua kesi mahakamani kupinga kitendo hicho kwa madai ya kufukuzwa kwao hakukuwa na msingi na kuna vitu havikuwa sawa.

“Kwa mujibu wa Katiba ya nchi yetu, chombo pekee chenye kutoa haki ni mahakama na hivyo kwa kuwa hawa wamekwenda mahakamani kupinga kufukuzwa kwao, jambo hili linatakiwa kuachwa kwanza hadi hapo mahakama itakaposema vinginevyo,” amesema Dk Tulia.

Huku wabunge wakiwa wanapiga makofi kwa nguvu kutoka pande zote, Spika alitangaza kuwa kuanzia leo anafunga mjadala wa kuzungumzia jambo la wabunge hao kutoka kwa mtu yeyote na kwamba kama kuna mtu anataka kujua kuhusu ubunge wao msemaji pekee atakuwa ni yeye Spika.

Wakati Spika akitoa kauli hiyo, kati ya wabunge 19 wanaotajwa, walikwepo 10 ambao baadhi yao mapema walishapewa maswali ya kuuliza mmoja akiuliza swali la msingi lakini watatu waliuliza maswali ya nyongeza.

Alhamisi iliyopita kikao cha juu cha maamuzi kuhusu masuala ya kinidhamu kutupilia mbali rufaa ya wabunge hao kupinga uamuzi wa Kamati Kuu ya chama hicho kuwafukuza uanachama Novemba 27, 2020.

Bajeti ya Fedha Kusomwa June 14 Siku ya Jumanne
PSPTB yazionya taasisi zisizotumia wataalam kwa kazi za ununuzi