Watanzania 16 wamehukumiwa kifungo cha Miezi Sita (6) jela au faini ya Tsh. 300,000 kila mmoja baada ya kukiri kuzamia Nchini Afrika Kusini kinyume na taratibu zilizowekwa na Idara ya Uhamiaji.

Wengine 14 wamehukumiwa kifungo cha miezi 18 au faini ya Sh 50,000 kila mmoja, baada ya kukiri kosa hilo.

Watuhumiwa hao walirudishwa nchini na kufikishwa Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu, ambapo walikiri mashtaka yaliyokuwa yanawakabili. Hakimu Agustina Mbando alitoa hukumu hiyo kutokana na makosa hayo kujirudia.

OSHA watia nanga na kampeni mpya Mwanza

Awali, Wakili wa Serikali, Godfrey Ngwijo, aliomba Mahakama kutoa adhabu kali na kusema utaratibu wa kutoka nje ya Nchi unafahamika.

Kwa mujibu wa Wakili huyo, washtakiwa waliondoka nchini Kinyume cha Kanuni za Uhamiaji namba 20 (3) (a) G.N namba 657 ya mwaka 1997 inayosomwa pamoja na kifungu namba 48 (2) ya Sheria ya Uhamiaji namba 54 iliyofanyiwa marekebisho mwaka 2016

Viongozi wa CCM waonywa tabia ya 'Majina mfukoni'
OSHA watia nanga na kampeni mpya Mwanza