Mchezaji aliyevunja mkataba na klabu ya Kinondoni Municipal Council (KMC) Abdul Halim Humoud, amejibu tuhuma za utovu wa nidhamu alizotuhumuwa na uongozi wa klabu hiyo wakati mkutano na waandishi wa habari uliofanywa juzi jumanne na katibu mkuu msaidizi Walter Harrison.

Houmud amesema tuhuma alizorushiwa na kiongozi huyo sio za kweli, na ameshangazwa na hatua ya kuzushiwa mambo mengi ambayo amedai hakuyafanya katika kipindi chote alichokuwa na klabu hiyo kinayoshiriki ligi kuu ya soka Tanznaia bara msimu huu wa 2018/19.

“Wameamua kunichafua jambo ambalo sijalipenda kabisa, nimefundishwa kutojipendekeza kwa mwalimu wala kutotoa rushwa hasa kutokana na baadhi ya viongozi kutaka asilimia kumi kwenye mshahara, nikaamua kujitenga pembeni, nina mke mzuri kuliko wachezaji wote pale KMC,” alisema.

Kwa upande wa uongozi wa KMC kupitia Ofisa habari Anwar Binde, umesema kuwa Humud anapaswa atambue kuwa uongozi umesimamia kweli kwa kuwa ushahidi upo wa maandishi pamoja na wake ambao walishawishiwa wapo.

“Asitafute huruma kwa sasa, kama anataka haki basi aende mahakamani kwa kuwa ushahidi upo na KMC ni taasisi inayojiendesha kwa utaratibu, masuala ya malipo kumbukumbu zipo za kila mchezaji iwe alilipwa pesa taslimu ama alilipwa benki,” alisema

Uongozi wa KMC uliamua kumruhusu Humud kuwa mchezaji huru baada ya yeye mwenyewe kuomba iwe hivyo kutokana na kile kilichoelezwa ni utovu wa nidhamu alioufanya ndani ya klabu ikiwa ni pamoja na kusahau vifaa vya michezo Dar es Salaam wakati timu ilipocheza na Coastal Union pamoja na kuwasumbua wake wa wachezaji wenzake.

Mahakama yamkalia kooni Mbowe, yatoa maagizo mazito
Serikali yawataka wakulima wa zao la Korosho kuwa wavumilivu