Uongozi wa Mabingwa wa Soka Tanzania Bara Simba SC, wameamua kufanya kweli baada ya kuwashushia wachezaji wao basi lingine aina ya TATA Marcopolo (New Model) kwa ajili ya shughuli za safari za ndani ya nchi.

Siri za uwepo wa basi hilo zilianza kuvuja kupitia mitandao ya kijamii jana Alhamis (April Mosi), ambapo picha zineonesha kwa sasa linaendelea kuwekewa ‘Stika’.

Kabla ya kuvuja kwa siri hizo, Simba SC walikua wanatumia basi aina ya Yutong walilokabidhiwa na wadhamini wao wa zamani kampuni ya bia nchini TBL mwaka 2012, na kudumu nalo mpaka leo hii.

Basi jipya la klabu hiyo aina Tata Marcopolo linamuonekano maridadi na tayari lilianza kubandikwa stika jana mchana zenye nembo za wadhamini.

Wakati gari hilo likiwa katika hatua za mwisho kukamilika, Uongozi wa klabu ya Simba tayari umetangaza kuliuza gari yao ya zamani aina ya Yutong.

Matola: Matokea kesho lazima
Ijumaa Kuu: Wakristo watakiwa kufuata sauti ya Mungu