Mke wa mwimbaji Mashuhuri Duniani Justine Bieber, Hailey Bieber amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu changamoto yaki afya iliyomkabili mwezi uliopita, ambayo ilimfanya moja kwa moja afikiri kuwa amepata ugonjwa wa kiharusi.

Utata wa kukumbwa na ugonjwa wa Kiharusi kwa Hailey, uliishia hospitalini ambako madaktari walibaini kuwa alikuwa na tundu kwenye moyo wake.

Kwa mujibu wa ripoti za TMZ inaelezwa kuwa, Hailey alikimbizwa hospitali baada ya kupata dalili zinazofanana na kiharusi na hata baadae madaktari kubaini kuwepo kwa damu iliyoganda kwenye ubongo wake.

TIA, tatizo linalofahamika kama kiharusi kidogo (a mini-stroke) jambo lililorandana na mawazo yake ya awali punde baada ya kuanza kuumwa.

Baada ya kuzungumzwa mengi kuhusu afya ya mrembo huyo, hatimaye Hailey ameamua kujitokeza hadharani na kueleza kwa undani zaidi hali halisi ilivyokuwa.

Hailey amesema alihisi “hisia za ajabu” katika mkono wake wa kulia akiwa nyumbani na Justin, na ncha za vidole vyake zikafa ganzi. Ghafla, hakuweza hata kuongea.

Alikimbizwa hospitali kwa gari la wagonjwa, na hakika kulikuwa na dalili za kiharusi, ikiwa ni pamoja na kuinamia upande wa kulia wa uso wake.

Ganzi na kukata kauli vilikuja kwa haraka, na ni wazi madaktari walikuwa na wasiwasi, kutokana na kuwa awali haukujulikana ni nini kilisababisha, lakini fikra za awali zilielekea kwenye tatizo la Covid ambalo Hailey alilipata siku za hivi karibuni yeye pamoja na mumewe Justin Bieber.

Mwanzoni walihisi kuwa hiyo inaweza kuwa sababu, anasema pia alikuwa amebadilisha vidhibiti vyake vya uzazi (Birth control) bila kushauriana na daktari wake hivyo kuna muda fikra zilimpeka kwenye kuhisi kuwa pengine hilo ni kosa lililopelekea kupatwa na hali hiyo.

Baada ya uchunguzi wa kina wa madaktari waliokuwa wakimpatia matibabu, hatimaye Hailey alibainika kuwa na kitu kiitwacho PFO kwa lugha ya kitabibu, yaani tundu/mwanya mdogo kwenye moyo wake.

Mrembo huyo mwenye umri wa miaka 25 alifanyiwa upasuaji ambao ulikwenda vizuri na kumfanya walau kurejea kwenye hali yake kawaida.

Hailey anasema amekuwa akitumia dawa za kusaidia damu kutiririka vizuri kwenye mishipa (Blood thinners) kila siku tangu tukio hilo ili kuepuka changamoto hiyo kujirudia tena, na kuweka wazi kuwa anashukuru madaktari wake waliweza kubaini sababu na sasa wanaweza kuendelea na shida nzima.

Simulizi: Madeni yalivyonitumbukiza kwenye umaskini
Tems aangukia mikononi mwa Future na Drake