Serikali imeweka mikakati ya kuliongezea thamani zao la dagaa pamoja na kutafuta suluhu ya upungufu wa malighafi ya samaki viwandani.

Akizungumza wakati wa mkutano na wadau wa Sekta ya Uvuvi wanaohusika na uchakataji wa minofu ya samaki na wavuvi kutoka mikoa ya Kanda ya Ziwa Victoria ambayo ni Mwanza, Kagera, Mara, Geita na Simiyu, Naibu Waizri wa Mifugo na Uvuvi Abdallah Ulega amesema, serikali imejipanga kuipa thamani uvuvi wa dagaa ili kuongeza uwekezaji wa zao hilo.

“Tunataka tupate vichanja vya kutosha katika kuanika dagaa sio dagaa wanamwagwa tu inatakiwa wawekwe kwenye Vichanja,” Amesema Waziri Ulega.

Aidha amehaidi Wizara kufanya mazungumzo na Benki ya Maendeleo ya Kilimo (TADB) na wadau mbalimbali ili kuwekeza katika uvuvi wa dagaa na kupanua wigo wa zao hilo.

Akitaja faida za zao hilo Naibu Ulega amesema wigo wa soko la dagaa ukipanuka zaidi inaleta faid hata ya utatuzi wa tatizo la utapiamlo kwakuwa dagaa wana madini ya kutosha na kushauri viwanda kuendeleza uchakataji wa dagaa na kuuza nje na ndani ya nchi, pia uvuvi huo huleta fursa za ajira na kupelekea kuku kwa pato la Taifa.

Hali kadhalika Naibu Ulega amewahasa wamiliki wa viwanda vya kuchakata minofu ya samaki kuhakikisha wanawalipa wavuvi stahiki zao kwa wakati ili waweze kuendelea kufanya nao biashara ya kuwauzia samaki kutokana na malalamiko kutoka kwa baadhi ya wavuvi kudai kuwa wamekuwa hawalipwi kwa wakati.

Nao baadhi ya uvuvi wakichangia katika mkutano huo wameiomba serikali iwasaidie katika utoaji wa taarifa ya bei elekezi ili kupunguza kubadilika badilika kwa bei za samaki zinazonunuliwa viwandani, lakini pia upatikanaji wa dhana za uvuvi na kuthibiti upatikanaji wa nyavu zisizotakiwa.

Kwa Mwaka wa fedha 2020/2021 kupitia Sekta ya Uvuvi wamefanikiwa kukusanya Shilingi Bilioni 22.6 ambapo serikali ilipanga kukusanya Shilingi Bilioni 33 na kwamba asilimia 80 ya mapato hayo yametokana na Ziwa Victoria.

Simba SC yaivutia kasi KMC FC
Prince Dube hatarini kuikosa Simba SC