Mbunge wa Mtera, Livingstone Lusinde maarufu Kibajaji, amemtaka Mbunge wa Kigoma Mjini, Zitto Kabwe, kuacha kutumia siasa kama zilizokuwa zikifanywa na aliyekuwa Mwenyekiti wa Chama cha DP, marehemu Mchungaji Christopher Mtikila za kushinda mahakamani kufungua kesi.

Amesema hayo katika mkutano wa wabunge wa Chama Cha Mapinduzi (CCM) na waandishi wa habari kuhusu kauli ya Zitto kuwa Muswada wa Marekebisho ya Sheria ya Vyama vya Siasa ikienda bungeni itapita kwa sababu wabunge wa CCM wengi ni makasuku.

“Zitto sasa hivi anachukua ‘style’ za Mzee Mtikila za kushinda Mahakamani badala ya kushinda kutafuta hoja na watu wake wa Kigoma, Yaani yupo ACT Wazalendo lakini akili anazotumia ni za hayati Mtikila, nadhani mke wa Mtikila kama kungekuwa na sheria ya kusimamia stahiki za mumewe ana uwezo wa kumshtaki Zitto ili aweze kumlipa fidia kwa kutumia jina la mumewe yaani Zitto Mtikila,” amesema Lusinde

Hata hivyo, kuhusu kauli ya Zitto ya kuwaita wabunge wote wa CCM ni makasuku, Lusinde amesema kuwa kazi ya bunge si ya kubeza, iwe mbaya au nzuri ndiyo kazi ya Bunge.

 

Shule iliyoathiriwa na bomu Kagera yapata msaada
Ndugai amtumia ujumbe Tundu Lissu, 'Unatakiwa urudi haraka'

Comments

comments