Nchi Uganda nje kidogo ya jiji la kampala anaishi Mariam Nabatanzi, Mwanamke anayeweza kutajwa kuwa miaongoni mwa waliozaa watoto wengi zaidi duniani, ambapo akiwa na umri wa miaka 38 tu amebahatika kupata watoto 44 aliowazaa yeye mwenyewe.

Watoto wote alionao ni kutotka kwa baba mmoja, hadi sasa walio hai ni 39,wasichana 15 na watoto wavulana ni 24, ambao wote anaishinao nyumbani kwake na anawasomesha shule japo kwa tabu kwani hujikuta anakosa ada za shule.

Kwa mujibu wa Mariamu haliyake ya kushika mimba kwa urahisi mwanzoni haikumshangaza na alifurahia, ” mwanzo nilipata pacha, nikashika minba tena na kupacha mara ya pili na pacha marayatatu nikafurahi lakini nilipopata pacha tena ilikuwa ya watoto wanne na niliendelea kuzaa hadi sasa wamefika 44″  ameeleza Mariam

Jambo la kustaajabisha ni kwamba baada ya kuzaa mtoto wa mwisho aliyenaye miaka miwili iliyopita, mumewake ameamua kumkiambia kwani aliona majukumu ya familia yanamshinda na mkewe anauwezo wakuendelea kuza.

Kutokana na idadi hiyo ya kuwa na watoto wengi imembidi kununua daftari la majina ambalo huwaita kila siku, na kunawengine ameamua kuwapatia majina ya watu maarufu, mtoto wake mkubwa ana miaka 24 na mdogo ana miaka 2, watoto wote alijifungua kwanjia ya kawaida isipokuwa wamwisho amejifungua kwa upasuaji kwani alikuwa na uzito wa zaidi ya kilogram 7.

Kwakuwa Ng’ombe haelemewi na nundule, Hivi sasa mariam yeye ndiye mama na baba wa watoto wake ambao wamegeuka kuwa rafiki zake, na anatengeneza matofali ya ujenzi na kuyauza ili kukidhi mahitaji ya watoto wake hasa chakula na elimu.

licha ya kuwa na watoto wote hao ameeleza kuwa anasumbuliwa na wanaume wanaotaka awazalie nawao watoto, lakini yeye hakubaliani na kuzaa tu anahitaji mwaume atakayeweza kuwalea watoto wake na wakaishi kwa pamoja.

Kwa mujibu wa wataalam wa Afya nchi Uganda wamesema kuwa nikawaida kwa mwanamke kuzaa kama alivyo zaa Mariam, lakini siokweli kama mariam dawa za kupanga uzazi zimemkataa kama alivyowahi kuambia katika kituo kimoja cha Afya.

 

Habari kubwa katika magazeti ya Tanzania leo Februari 17, 2019
Hapo kale: Mambo sita ya Malkia Elizabeth II usiyoyajua