Shirikisho la Riadha Duniani limeitaka Urusi, ifikapo mwishoni mwa wiki, kujibu tuhuma za kuhusiaka na dawa za kusisimua misuli.

Rais wa Shirikisho la Riadha Duniani IAAF Sebastian Coe ametoa agizo hilo baada ya ripoti ya WADA.

Amesema shirikisho hilo litaangalia njia mbalimbali kufuatia ripoti iliyotolewa Shirikisho la kupambana na matumizi ya dawa ya kusisimua misuli WADA kuhusiana na wanariadha wa Urusi na matumizi ya madawa hayo.

Lord Coe, amesema amewakata kwa haraka wajumbe wa mamlaka iliyopo kufikiria kuliwekea vikwazo shirikisho la riadha nchini Urusi ikiwemo kusitishwa uanachama wake:

“nimeliomba shirikisho la riadha nchini Urusi kujibu tuhuma hizo ifikapo mwisho wa wiki hii. Nimewaomba wajumbe wangu kukutana siku ya Ijumaa. Inategemea tutakachokisikia kama jibu la tuhuma hizo, tutaangalia njia mbali mbali ikiwemo vikwazo.”

Rais huyo pia amesema hatasita kupambana na mapungufu yoyote yatakayojitokeza kama taasisi hiyo.

“Iwapo kuna somo la kujifunza, iwapo kuna mapungufu katika mfumo wetu, basi sharti nirekebishe hali hiyo. Tutajitathmini upya, hatufichi katika hilo. Nataka kuona mchezo ambao uko wazi na unaowajibika. Na nitafanya kila niwezalo kufanikisha hilo. Ingawa hiyo haitakuwa ni safari nyepesi. Hii itakuwa ni kazi ngumu.”

Wakati huo huo, hatua hiyo ya Urusi kuzuiwa kushiriki katika mashindano ya Olympic hapo mwakani imepokelea kwa hisia tofauti wa raia wa nchi hiyo. Hawa ni baadhi yao:

Victoria Beckham aonesha mapenzi yake Beckham kwenye jukwaa la ‘Glamour Awards’
Ronaldo Azindua Filamu Yake Jijini London