Uongozi wa klabu ya Rangers ya Scotland umefanikiwa kumsainisha mkataba wa kudumu mshambulaiji wa pembeni kutoka nchini Romania, Ianis Hagi.

Hagi mwenye umri wa miaka 21 alihamia Ibrox Stadium kwa mkopo mwezi Januari mwaka huu akitokea KRC Genk ya Ubelgiji, na alitarajiwa kuwepo klabuni hapo hadi mwishoni mwa msimu huu, kwa mujibu wa makubaliano ya pande hizo mbili.

Hata hivyo klabu ya Rangers ilikuwa na chaguo la kumsajili moja kwa moja baada ya kumalizika mkataba wa mkopo na mchezaji huyo, endapo wataridhishwa na kiwango chake, na imethibiti wamependezwa na uwezo aliouonyesha.

Mshambuliaji huyo tayari ameshatumikia timu yake ya taifa ya Romania katika michezo kumi, akitokea kucheza katika timu za vijana mara mbili ametajwa kuwania tuzo ya mchezaji bora chipukizi barani Ulaya (European Golden Boy).

Hagi, mtoto wa nyota wazami wa FC Barcelona na Real Madrid, Gheorghe Hagi, alifunga mabao matatu katika michezo kumi na mbili akiwa na Rangers, ikiwa ni pamoja na magoli yake mawili katika hatua ya 32 ya Europa League dhidi ya Braga kabla ya ligi ya Scotland kusimamishwa mnamo Machi 13.

Ndalichako: Marufuku wanafunzi kwenda shule na Tangawizi, malimao, na spriti
Shah Mjanja: Ligi kuchezwa mkoa mmoja sawa na kucheza ugenini