Serikali ya Italia na Maaskofu wa Kanisa Katoliki wamesaini makubaliano ya kuruhusu Ibada pamoja na mikusanyiko ya kidini kama harusi kuanzia Mei 18, 2020 huku kanuni za usalama zikizingatiwa.

Ambapo mapadri na waumini watakiwa kuvaa barakoa na vitakasa mikono kuwekwa mlangoni mwa Kanisa na vifaa vyote vinavyotumika ibadani kusafishwa baada ya misa kumalizika.

Vilevile, waumini wametakiwa kuzingatia umbali wa mita moja na mapadri wameelekezwa kutoa Ekaristi Takatifu wakiwa wamevaa glovu na kuhakikishi hawagusi mikono ya wapokeaji.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Luciana Lamorgese amesema makubaliano kama hayo yatasainiwa na madhehebu mengine ya dini siku za hivi karibuni.

Italia ilipiga marufuku ibada tangu Machi 9, 2020 kufuatia mlipuko wa #COVID19. Jumla ya visa 215,858 na vifo 29,958 vimerekodiwa nchini humo na waliopona ni 96,276.

Wachezaji Tanzania bara waomba wiki mbili
WHO: Watu milioni 44 wanaweza kuambukizwa corona Afrika