Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Ajira na wenye Ulemavu Jenista Mhagama, ameeleza uwepo wa ibada ya kuwaombea Hayati Baba wa Taifa Mwl. Julius Nyerere, Benjamin Mkapa na Hayati Dkt. John Magufuli ikiwa ni sehemu ya kuwaenzi kuelekea kuhitimishwa kwa mbio za Mwenge wa Uhuru 2021.

Amesema kuwa kuna umuhimu wa ibada hiyo, kwa kuzingatia michango ya viongozi hao katika Taifa na kusema ni sehemu ya kuwaenzi na kuonesha heshima kwa namna walivyolitumikia Taifa.

Amesema kuwa, Kanisa kwa kushirikiana na kamati ya maandalizi wana jukumu la kuiandaa ibada hiyo ya kipekee kulingana na heshima kubwa ya viongozi hao katika Taifa na kuonesha tunatambua michango yao kwa matendo.

Mbio maalum za Mwenge wa Uhuru 2021, zitahitimishwa Oktoba 14 wilayani Chato mkoani Geita.

Watanzania waombwa kuacha kukumbatia tamaduni za kigeni
Wizara ya Afya yafanya mabadiliko ya ujenzi