Ibada ya Hijjah nchini Saudia imefika kilele chake huku takribani Waislamu milioni 1.5 wakikongamana katika mlima Arafat ili kufanya maombi ya siku nzima, mbali na kusoma Quran.

Mahujaji hao walikongamana katika mlima huo wakati wa machweo ambao uko takriban kilomita 15 kutoka mji wa Mecca

Waislamu wanaamini kwamba mtume Muhammad alitoa hotuba yake ya mwisho katika eneo hilo.

Nguzo ya Hijjah ni mojawapo ya nguzo tano za kiislamu ambayo Waislamu hutakiwa kuitekeleza ijapokuwa mara moja , Siku ya Jumamosi imeelezwa kuwa kiongozi mkuu wa dini nchini Saudia Abdul Aziz al-Sheikh hakuweza kutoa hotuba yake ya kawaida kwa mara ya kwanza katika kipindi cha miaka 35 kutokana na sababu za matatizo ya kiafya

Hillary Clinton Augua Ugonjwa wa Homa ya Mapafu, Donald Trump Achekekelea
Ndesamburo adai jahazi la nchi linazama, Ole Sendeka ajibu mapigo