Watu 24 wamepoteza maisha na makumi wamejeruhiwa baada ya mtu mmoja kufyatua mabomu ya kujitoa mhanga katika tukio la mazishi nchini Afghanistan.

Mtu huyo anayesadikika kuwa ni mpiganaji wa kundi la kigaidi la ISIS alifyatua mabomu hayo jana, Mei 2, 2020 katikati ya ibada ya mazishi katika Wilaya ya Kuz Kunar.

Msemaji wa Gavana wa Jimbo la Nangarhar, Attaullah Khogyani amesema kuwa waombolezaji walikuwa wamekusanyika kumzika Kamanda wa Jeshi la Polisi wa Wilaya hiyo, Shaykh Akram aliyefariki baada ya kupata mshtuko wa moyo, Jumatatu usiku kufuatia mlipuko wa mashambulizi ya mabomu.

Kundi la ISIS limekiri kutekeleza mashambulizi hayo kupitia ujumbe uliosambazwa kwenye telegram.

“Mwana Jihad, Abdallah al-Ansari amepiga walinzi wa Afghan na washirika wao kwa kutumia mkanda wa mabomu ya kujitoa mhanga… ameua na kujeruhi watu 100 wasiowaamini,” imeeleza taarifa ya ISIS.

Hivi karibuni, Jeshi la Marekani na Afghanistan kwa pamoja yameshambulia vikali wapiganaji wa ISIS. Mashambulizi dhidi ya ISIS pia yalitekelezwa na wapiganaji wa Taliban.

Wapiganaji wa Taliban wao walisitisha mashambulizi dhidi ya vikosi vinavyoongozwa na Marekani, baada ya kusaini makubaliano na Marekani Mwezi Februari mwaka huu.

Makubaliano hayo yanaonesha mwanga wa kuwepo kwa mazungumzo kati ya Taliban na Serikali ya Kabul.

Visa vya corona vyafika 737, visa vipya 22 vyabainika – Kenya

Ayoub Lyanga: Young Africans hawatimizi ahadi, nitakwenda Serbia

Waumini 44 wa parokia moja wafariki kwa corona, mchungaji aeleza
Luc Eymael kuamua hatma ya Kaseke