Kocha wa AS Vita ameng’aka mbele ya waandishi wa habari na kutamka kwamba: “Mwambie basi Rais anifukuze.” Ibenge ametoa kauli hiyo ikiwa ni hasira ya kuulizwa kila mara hatma yake na timu yake baada ya kipigo cha bao 1-0 la Simba kwenye uwanja wa nyumbani.

“Mimi ni kocha nawajibika kwenye kilichotokea, mwambieni Rais wangu anifute kazi,”aling’aka Kocha huyo ambaye waandishi wengi walikosoa staili yake ya uchezaji pamoja na kikosi chake cha kwanza.

“Waandishi mnakuja mazoezini mnaona viwango vya wachezaji mnasifia tu, kazi ya Kocha haiishi hapo kuna mambo mengi ya kuzingatia,nyie siyo makocha,”aliongeza.

Kocha huyo alisema kwamba mabadiliko matano aliyoyafanya kipindi cha pili yaliongeza uhai kwenye kikosi chake lakini wachezaji wake wanahitaji muda mwingi wa kucheza kutokana na hofu ya Corona.

Mashabiki wengi wa Vita hawakutegemea kilichoitokea timu yao na kupoteza nyumbani dhidi ya Simba ambao msimu mmoja uliopita waliwapiga mabao 5-0.

Chanzo: Mwanaspoti

Tanzania, EU zasaini mkataba wa Bil. 307.9
Watu 60 wafariki baada ya boti kuzama