Kocha Mkuu wa Mabingwa wa Soka nchini Sudan Al Hilal Florent Ibenge amemshauri Kocha wa Young Africans Nasreddine Nabi, kutokana na maboresho aliyoyafanya kwenye kikosi chake kupitia Dirisha Dogo la Usajili.

Young Africans imesajiliwa Wachezaji wanne ambao ni mlinda Lango Metacha Mnata (Tanzania), Kennedy Musonda (Zambia), Beki Mamadou Doumbia (Mali) pamoja na Kiungo Mudathir Yahya Abbas (Zanzibar).

Ibenge amesema kutokana na maboresho hayo, Kocha Nabi hana sababu ya kushindwa kupata matokeo ya ushindi katika Hatua ya Makundi ya Kombe la Shirikisho Barani Afrika msimu huu 2022/23.

Amesema Young Africans imefanya maboresho ya kimsingi kwenye kikosi chake kuelekea Mshike Mshike wa michuano hiyo ya Barani Afrika, hivyo anaamini watapambana na kuwafurahisha Mashabiki wao na Watanzania kwa ujumla.

“Wamesajili vizuri kutokana na mahitaji ya kikosi chao, ukiangalia wamemsajili Beki, Mshambuliaji na Kiungo mmoja kwa lengo la kuziba mianya kabla ya kuelekea kwenye Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika mwezi ujao.”

“Sidhani kama kutakuwa na sababu nyingi za wao kushindwa kupata matokeo mazuri katika michezo ya hatua ya Makundi, kwa maana wachezaji wanapata muda wa kuzoeana kabla ya kuelekea kwenye Michuano hiyo.”

“Kama wakiongeza umakini wanayo nafasi ya kufika mbali zaidi kwenye michuano hiyo, ambayo bado inaendelea kubeba sifa ya ushindani na upinzani mkubwa kutokana na timu zilizofuzu kuwa na uwezo wa kupambana katika michezo ya nyumbani na ugenini.”

Katika Hatua ya Makundi Kombe la Shirikisho Barani Afrika, Young Africans imepangwa Kundi D sambaba na TP Mazembe (DR Congo), Real Bamako (Mali) na AS Monastril (Tunisia).

Jinsi ya kumthibiti mama mkwe mvunja ndoa
Kiwango cha Metacha chamkuna Nabi