Kiungo mshambuliaji wa klabu ya Simba, Ibrahim Ajib ameanza majaribio yake vizuri baada ya kupiga bao akiwa mazoezini na klabu ya Golden Arrows ya Afrika Kusini.

Ajib ambaye aliondoka nchini bila kupata baraka za uongozi wa klabu ya Simba ameanza majaribio hayo jana katika klabu hiyo ya Ligi Kuu Afrika Kusini.

Meneja wake, Juma Ndambile amesema Ajib ameanza vizuri kwani pamoja na bao hilo, alicheza vizuri.

“Walifanya mazoezi mengine ya kawaida, baadae kocha akaamua wacheze full game. Nafikiri alitaka kumuona.

“Ajib alicheza vizuri kwa kweli, amefanikiwa pia kufunga bao zuri kabisa,” alisema.

“Kesho (leo) ataendelea na majaribio yake na itakuwa hivi kwa siku kadhaa zijazo.”

Awali Ndambile alisema Ajib akimalizana na Arrows na kama mambo hayatakuwa mazuri, atafunga safari hadi katika kikosi cha daraja la kwanza cha Amazulu ambako pia amepewa nafasi ya kufanya majaribio.

Didier Deschamps Ataja Jeshi La Wenyeji - Euro 2016
Sasa Ni Makundi Manne, Sio Mawili Tena

Comments

comments