Simba imejiongezea alama tatu za Ligi Kuu Bara baada ya kuitwanga Ndanda FC kwa bao 1-0.
Licha ya Simba kuchezesha wachezaji wote saba katika kikosi cha kwanza wanaotokea katika mataifa matano ya kigeni, shujaa wao ameibuka kuwa Ibrahim Ajib aliyefunga bao pekee katika dakika ya 81.
Kama utajumlisha wachezaji hao kutokea katika mataifa matano ya kigeni yaani Ivory Coast, Kenya, Zimbabwe, Uganda na Burundi pamoja na Tanzania, maana yake Simba ilichezesha wachezaji kutoka mataifa sita tofauti katika wachezaji 11 walioanza katika kikosi cha kwanza.
Ushindi huo ulikuwa mgumu kwa Simba ambayo ililazimika kufanya kazi ya ziada kutokana na kutocheza kwa kiwango cha juu sana huku Ndanda wakitoa upinzani mkali.
Anagalau baada ya kupatikana kwa bao hilo, Simba walizidi kuiandama Ndanda wakitaka kupata bao la pili, lakini haikuwezekana.
Kocha Dylan Kerr alipanga kikosi chenye wachezaji wote saba wa kigeni ambao wanaruhusiwa na Shirikisho la Soka Tanzania na kufanya aweke rekodi mpya ya kikosi kuanza na wachezaji wote wageni.
Wageni walioanza katika kikosi cha leo cha Simba ni Vicent Agban (Ivory Coast), Emiry Nimuboma (Burundi), Justice Majabvi (Zimbabwe),  Paul Kiongera (Kenya) na Hamisi Kiiza, Brian Majwega (wote Uganda).

Ligi Ya England Kuendelea Wikiendi Hii
Hoteli za Double Tree, Slipway na Nyumba ya Kigogo Huyu Vyasombwa na 'Bomoabomoa'