Kiungo Mshambuliaji wa Simba, Ibrahim Ajibu amekatwa shilingi 200,000 katika mshahara wake mwisho wa mwezi Mei, kama adhabu ya kushindwa kufika kambini kwa wakati juma lililopita.

Awali kiungo huyo alifukuzwa kambini na kocha mkuu wa Simba, Sven Vandenbroeck na kutakiwa kuripoti kambini jana Jumatatu, kufuatia sababu alizozitoa kwa kocha huyo kutoakua na mashiko.

Mwishoni mwa juma lililopita kocha Sven Vandenbroeck alithibitisha kumfukuza kambini kiungo huyo, kwa kusema hakufika kwa wakati kama walivyoagizwa wachezaji wote kwa ajili ya kuanza maandalizi ya kuendelea na ligi kuu.

Hata hivyo Jana Jumatatu Ajibu alifika kambini, kisha akawa na mazungumzo mafupi na kocha Vandenbroeck na baadae aliruhusiwa kuwa miongoni mwa  wachezaji ambao watafanya mazoezi jioni.

Katika mazoezi hayo Ajibu alikutana na cha moto kwani alikuwa akikimbizwa mbio za kuzunguka uwanja huku Sven akiwa anamsimamia.

Wakati Ajibu akiwa anakimbia mbio za kasi na pole pole akizunguka uwanja, Sven alikuwa akimsimamia huku wachezaji wengine wote wakiwa kati kati ya uwanja  wakifanya mazoezi ya kawaida.

Mazoezi hayo ya kawaida kwa wachezaji wengine yalikuwa yakisimamiwa na kocha wa viungo, Adel Zrane aliyekuwa sambamba na kocha msaidizi Selemani Matola.

Ajibu hakuwa anakimbia mwenyewe bali alikuwa na wachezaji wengine, Rashid Juma na Francis Kahata ambaye nae ndio alikuwa anafanya mazoezi ya kwanza yale ya uwanjani akiwa na kikosi hiko tangu aliporejea nchini.

Sven alionekana kumkazania  Ajibu akimtaka akimbie kwa kasi kama vile ambavyo alikuwa.

Kai Havertz amnyima usingizi Solskjaer
Ripoti: Kilichotokea baada ya Trump kutishia kutumia jeshi kuzima maandamano