Mwanachama mkongwe wa klabu ya Young Africans Ibrahim Omary Akilimali amefariki dunia leo asubuhi ya Desemba 14, katika Hosptali ya Bagamoyo baada ya kuugua Kwa muda mrefu.

“Nimepokea simu leo asubuhi kutoka kwa ndugu wa Mzee Akilimali akinijulisha kuhusu msiba huo. Alisema atanipa taarifa zaidi baada ya kufika Bagamoyo,” amesema Ofisa Habari na Mawasiliano wa Young Africans, Hassan Bumbuli.

Akizungumzia msiba huo, Mwenyekiti Umoja wa Tawi la Young Africans kwa Mtogole, Waziri Ramadhani amesema marehemu Akilimali ambaye aliwahi kuwa katibu wa Baraza la Wazee Young Afrucans, atazikwa kesho saa 10 katika Makaburi ya Tandale kwa Mtogole.

Mara baada ya taarifa za msiba wa Mzee Akilimali ambaye alikuwa mwanachama wa Young Africans tangu mwaka 1972 na ambaye amejipatia umaarufu mkubwa kutokana na misimamo yake ndani ya klabu hiyo, wadau mbalimbali wa michezo wametuma salamu za rambirambi.

Mmojawapo ni msemaji wa klabu ya Simba, Haji Manara ambaye katika ukurasa wake wa Instagram ameandika, “Tumeondokewa na mwamba katika miamba ya kabumbu nchini.

Mzee wetu, baba yetu na mwenyekiti wa Baraza la Wazee Yanga, Ibrahim Akilimali katangulia mbele ya haki. Poleni familia, poleni sana Wanayanga, hakika huu ni msiba wetu sote na tutashiki kikamilifu kwenye majonzi haya.

Zanzibar: Daktari kizimbani kwa kuomba rushwa ya ngono kwa Mjamzito
Video: Herry Mzozo 'atema cheche' Tshabalala masikini,Msuva,Sureboy kasajiliwa kwa 150,000