Bondia nyota wa Tanzania Ibrahim Class ametamba kumchapa mpinzani wake Gustavo Pina Melgar kutoka Mexico katika pambano la kimataifa lililopangwa kufanyika Ijumaa (Septemba 30) kwenye ukumbi wa Mlimani City.

Pambano hilo limeandaliwa na kampuni ya MO Boxing, ikiwa ni mara ya kwanza kwa kampuni hiyo chini ya mfanyabiashara maarufu, Mohammed Dewji.

Akizungumza na Dar24 Media, Bondia Class amesema kuwa baada ya kukaa nje ya ulingo kwa muda mrefu, ameamua kurejea kwa kasi kwa lengo la kutwaa mikanda mbalimbali ya ngumi za kulipwa nchini.

Amesema kuwa amejiandaa vyema kwa ajili ya pambano hilo na hatamdharau mpinzani wake kwani anaamini naye amekuja kwa ajili ya ushindi.

“Najua Melgar ni bondia mzuri lakini si kwa kufikia kwangu, nimejiandaa vyema na nimuonyesha jinsi gani Tanzania ina mabondia wazuri na wenye vipaji vikubwa,” amesema Class.

Kwa upande wake, Melgar amesema kuwa amekuja kusaka ushindi ili kuboresha rekodi yake katika ngumi za kulipwa.

Mratibu wa pambano hilo kutoka MO Boxing Ahmed Seddiqi amesema kuwa maandalizi yamekamilika na kutakuwa na mapambano sita ya utangulizi.

Serengeti Girls kuonja tamu, chungu za VAR
Waandishi wa habari, Mashabiki wanyooshewa kidole