Inter Millan waliibuka na ushindi wa mabao 3-2 dhidi ya wapinzai wao wa jadi Ac Millan katika mchezo wa ligu ya Italia Serie A huku mshambuliaji Mauro Icardi ambaye ni nahodha wa klabu hiyo akipiga Hat-trick katika mchezo huo.

Dakika 28 tu za mwanzo Icardi alionesha makucha yake baada ya kufunga bao la kwanza lililodumu hadi mapumziko, lakini Ac Millan walirudi kipindi cha pili na kusawazisha kupitia kwa Susso.

Mauro Icardi tena dakika ya 68 aliongeza la pili kabla ya Millan kuchomoa dakika ya 81 kupitia kwa Giacomo Bonaventura na wakaamini mpira unaweza isha kwa suluhu lakini Icardi tena dakika ya 90 akafunga bao kwa mkwaju wa penati na kuifanya Inter Millan kushinda 3-2.

Kwa matokeo hayo sasa Ac Millan wanashika nafasi ya 10 na alama zao 12 huku Inter Millan wakibaki katika nafasi yao ya pili wakiwa wamejikusanyia alama 22 msimu huu.

Mchezo huo ulikuwa na msisimko wa kipekee ukihudhuliwa na mashabiki wengi kutokana na uwekezaji mpya ulifanywa na timu zote mbili zinazomilikiwa na wawekezaji kutoka China.

Wasira aunga mkono Serikali kukoselewa
JPM amtumbua Hassan Kibelloh, afanya uteuzi upya