Mwendesha Mashtaka Mkuu wa Mahakama ya Kimataifa ya Uhalifu (ICC), Karim Khan amesema ataomba majaji wa kesi dhidi ya mbabe wa kivita wa Uganda Joseph Kony, kuthibitisha mashtaka dhidi ya mtuhumiwa hata kama hatokuwepo Mahakamani.

Mahakama hiyo, ilitoa hati ya kukamatwa kwa Kony mwaka 2005 kwa madai ya uhalifu wa kivita na uhalifu dhidi ya binadamu, na Rais wa Marekani wakati huo, Barack Obama mwaka 2011 alianzisha kikosi kidogo cha wanajeshi kusaidia majeshi ya kikanda ili kumkamata.

Joseph Kony. Picha ya Guardian.

Kony, ni Kiongozi wa kundi la Lord’s Resistance Army (LRA), ambaye alianzisha uasi wa umwagaji damu zaidi ya miongo mitatu iliyopita, akitaka kulazimisha takwa lake mwenyewe aliloliita Amri Kumi za Mungu huko kaskazini mwa Uganda.

Van Gaal: Tupo hapa kucheza soka, hatugombani
Harry Kane kuivaa Marekani leo