Makamu wa Pili wa Rais Zanzibar, Balozi Seif Ali Iddi amesema hadi kufikia leo mei 27,2020 kuna jumla ya watu 134 wamethibithibitishwa kuumwa Corona Zanzibar, 115 wamepona na 19 bado wanaendelea na matibabu.

Akizungumza kwenye televisheni ya Taifa ya Zanzibar (ZBC) leo amesema kupungua kwa wagonjwa kumetokaana na kufuata maagizo ya viongozi wa juu wa kitaifa.

“Jumla ya wagonjwa 115 wamepona ugonjwa huu na mpaka sasa wamebakiwa wagonjwa 19 tu wanaopatiwa matibabu kwenye vituo vya kutibu wagonjwa hawa nchi nzima ” amesema Balozi Iddi.

Ikumbukwe kuwa mgonjwa wa kwanza wa Corona Zanzibar aligunduliwa mnamo mwezi Machi na tangu hapo kumekuwa na kambi maalum za kutibu wagonjwa wa corona visiwani humo.

Mkutano wa Baraza la Mawaziri SADC ngazi ya Makatibu wakuu umeanza kwa njia ya mtandao
Idris Sultani aachiwa kwa dhamana Kisutu