Idadi ya waliofariki katika ajali ya Lori iliyotokea mkoani Morogoro imezidi kuongezeka na kufikia 95 baada ya majeruhi mmoja aliyekuwa amelazwa katika hospitali ya taifa Muhimbili kufariki dunia jana jumamosi usiku.

Aidha, jana alasiri Hospitali hiyo ilipokea majeruhi mwingine kutoka Hospitali ya Mkoa wa Morogoro na kufanya idadi yao kuwa 21 lakini kwasasa wamebaki 20 baada ya mmoja kufariki jana usiku.

Ajali hiyo ilitokea Agosti 10, 2019 katika eneo la Msamvu baada ya Lori la mafuta kupinduka na kuwaka moto muda mfupi baada ya watu kuanza kuchota mafuta.

Akizungumza leo jumapili Agosti 18, 2019, mkuu wa kitengo cha mawasiliano wa Hospitali ya Taifa Muhimbili, Aminiel Aligaeshi, amemtaja aliyefariki dunia kuwa ni Rajabu Ally.

Hata hivyo, Aminiel amebainisha kuwa wagonjwa 20 bado wapo katika chumba cha uangalizi maalum (ICU), madaktari wanafanya kila jitihada kuokoa maisha yao.

Watu 63 wafariki dunia Afghanistan
NGO's 158 zaondolewa kwenye rejista ya Msajili