Wanafunzi 230 wa shule za msingi na sekondari mkoani kilimanjro wamekatisha masomo baada ya kubainika ni wajawazito tangu januari hadi Agosti, mwaka huu.

Kutokana na hali hiyo, serikali mkoani huo imeliagiza jeshi la polisi kuacha kufanya kazi kwa mazoea na kuhakikisha linawakamata watuhumiwa wote waliohusika kuwapa ujauzito wanafunzi hao na kuwafikisha mbele ya vyombo vya sheria.

Kauli hiyo imetolewa na mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro, Said  Meck Sadik, wakati wa sherehe za kuwapongeza na kuwakabidhi zawadi maofisa 34 wa jeshi la polisi waliohitimu kozi za uongozi jana.

Wanafunzi wa kike 238 katika kipindi hicho, wameshindwa kuendelea na masomo kutokana na kupata ujauzito wakiwa shuleni jambo ambalo ni hatari na tishio katiaka utoaji wa elimu bora kwa watoto wakike.

”Januari hadi mei mwaka huu tulikuwa na wanafunzi wajawazito 77, lakini ripoti ya agosti walipopimwa, tumekuta wameongezeka mpaka 238, jamani Taifa linapoteza wasomi”. alisema Said Meck Sadik mkuu wa mkoa Kilimanjaro.

 

 

Video: Kwanini uchumi wetu unakuwa lakini haupunguzi umaskini? - Prof. Ngowi
Prof. Mbarawa amteua Dk. Mgwatu kuwa Mtendaji Mkuu TEMESA