Idris na Wema Sepetu wameamuwa kuwaambia yote mashabiki wao kuhusu uhusiano wao na kile wanachokitarajia kutokana na uhusiano huo.

Leo, baba huyo mtarajiwa ameweka wazi umri wa ujauzito wa Wema hivyo kutoa picha ya muda wanaotarajia kumpokea duniani mtoto wao mpendwa.

Idris

“Yes very soon natarajia kupata mtoto kama miezi 6 au 7 ijayo,” Idris alikiambia kipindi cha Amplifaya cha Clouds Fm, hali iliyotafsiriwa kama Wema ana ujauzito wa miezi miwili hadi mitatu.

“Hatujui… mwenzangu anataka suprise, mimi nataka kujua kabla. Kwahiyo bado hatujafikia muafaka. Naogopa nisije kuwa nanunua vigauni akaja wa kiume,” aliongeza.

 

 

Membe azungumzia mpango wa kustaafu Siasa, aanza kuandika vitabu kama Sitta
Membe akaribishwa Chadema