Aliyewahi kuwa mshindi wa Big Brother Africa (BBA) na staa wa filamu ya kiumeni, Idris Sultan amefanikiwa kupita katika mchujo wa kushiriki filamu itayokwenda kwa jina la ”Ballin on the other side of the world”.

Itakayoongozwa na Harvey White na Sehemu kubwa ya filamu hiyo kufanyika katika mji wa New York.

Harvey White ni muongozaji mkubwa wa filamu kali na maarufu zinazopendwa duniani kote zikiwemo  ‘Think like a man 2’, ‘The wedding ringer’, na ‘king of the dance hall’.

Filamu hiyo inazungumzia maisha ya kijana wa Kikenya (Kunjan) ambaye wazazi wake ni waathirika wa uharifu.

Idris ‘King’ katika filamu hiyo atavaa uhusika wa kijana mcheshi na  mtukutu anayejishughulisha na makundi ya uhalifu lakini pia rafiki wa karibu wa Kunjan.

Mkurugenzi kampuni ya D Street, Dexter Davis ametoa nafasi kwa watanzania wenye vipaji kuijitokeza kuonesha vipaji vyao vya uigizaji filamu kwani hata baada ya kumpata Idris Sultan wanakusudia kufanya usaili zaidi kutafuta vipaji zaidi kutoka Tanzania.

 

Video: Cheyo awararua Lowassa na Sumaye, DCI awaanika vigogo wapya kwenda Keko
Urusi yadaiwa kudukua vitalu vya nyuklia vya Marekani