Msanii wa vichekesho, Idris Siltani amepata dhamana katika Mahakama ya hakimu mkazi Kisutu baada ya kutimiza masharti ya kuwa na wadhamini wawili na bondi ya millioni 15,000,000.

Msanii huyo amefikishwa Mahakama ya mkazi Kisutu leo Mei 27, 2020 ambapo anatuhumiwa kumiliki laini ya simu ya innocent Maiga huku Maiga akishindwa kuripoti mabadiliko ya laini yake .

Aidha washitakiwa hao wamesomewa mashitaka yao na wakili wa Serikali mwandamizi, Wankyo Simon, Matilda Mushi na Estazia Wilson mbele ya Hakimu Mkazi Mwandamizi, Rashid Chaungu.

Katika kesi hiyo ya jinai, inadaiwa ametenda kosa hilo kati ya Desemba 1, 2019 na Mei 19, 2020 maeneo ya Mbezi Beach Kinondoni ambapo alitumia kadi ya simu iliyomilikiwa na Innocent Maiga bila kuripoti kwa mtoa leseni.

Hata hivyo, Wakili wa Idris Sultan, Benedict Ishabakaki ameondolewa kumuwakilisha mshitakiwa huyo kwa sababu atatumika kama sehemu ya ushahidi wa upande wa Jamhuri kutokana na kushuhudia mshitakiwa wake akichukuliwa maelezo Polisi, hivyo anabakia mmoja ambaye ni Jebrah Kambole.

Idadi ya wagonjwa wa corona Zanzibar yapungua, 115 wamepona
Boti za Zanzibar I, II zasitisha safari baada ya kupata hasara