Mchekeshaji Idris Sultan ametumia ukurasa wake wa Instagram kumpongeza mwanamitindo Hamisa Mobetto kujiingiza kwenye muziki na kudai kuwa anamsapoti kwa uamuzi huo na anashangazwa na watu wanaomsema na kumkejeli kwenye hatua zake za utafutaji na kumshauri asikubali kukatisha kile anachokiamini yeye.

Idris amemshauri Hamisa na kumpa moyo kuwa ipo siku atakuja kufanikiwa na kuchukua matuzo makubwa kupitia muziki.

Hii imekuja baada ya muda mfupi tu Hamisa kuachia wimbo wake mpya ambapo baadhi ya watu wamekuwa wakitoa comment zao juu ya wimbo huo huku wengine wakikejeli kuwa Hamisa hajafanya vizuri.

“Naomba niwe kati ya wale wa kwanza kukusapoti ili ukija kuanza kuchukua matuzo usitusahau maskini wenzio. Mwanzo sio mwepesi ila kama msimamizi wa mpesa vodacom naweza sema yajayo yanafurahisha. Nitashangaa kuona watu wanakukejeli kwenye hii hatua yako katika upiganaji sijui wanataka ukatembee barabarani unauza nanilii sasa 😒.”

“Katika hatua za mafanikio jua sana kuchuja maneno. Kama kweli umedhamiria kufanya mziki basi kazaaa na unatoboa tu kwani hao wengine ni kina nani labda. Wengine tulianza hatukubaliki hata tutoe msaada wanguo zetu tutembee watupu ila unakaza tu na baada ya mda unaanza okota fan mmoja mmoja wawili mwishowe una mamilioni #Refuse To Stop” – Idris Slutan

Jana August 20, 2018 Hamisa Mobetto ameachia wimbo wake mpya unaokwenda kwa jila na Madam Hero.

 

 

 

Bobi Wine kutetewa na mawakili 24
RC Mwanri awaweka kikaangoni Maafisa Ustawi wa Jamii